Na. Mwl. Venance F.
Wanafunzi wa kidato cha sita 2017 mara baada ya kumaliza mtihani wao wa mwisho leo (Jumanne, tar. 9/5/2017) waliamua kuwashukuru na kuwaaga walimu wao. Walimu walitoa nasaha mbalimbali kwa wahitimu hao zoezi lilioenda sambamba na wanafunzi kuwalisha keki walimu wao kama ishara ya shukrani lakini pia Mkuu wa shule kwa niaba ya walimu wote aliwalisha keki wahitimu hao kama ishara ya kuwatakia mema na kukubari shukrani yao. Nimekuwekea hapa picha zinazoeleza tukio zima:
Wanafunzi wa Kidato cha Sita 2017 wakiwa wamekusanyika
katika ofisi ya
Mkuu wa Shule kusikiliza nasaha za mwisho
kabla ya kutawanyika kuelekea
mtaani
Afande nae akaamua kutwanga foto na wanafunzi
alioshiriki kuwasimamia
Mkuu wa Shule Madam, Lubasi pamoja na afande Lucy
wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
Mkuu wa Shule akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wahitimu kidato cha VI 2017
Wahitimu waliandaa keki kwa ajili ya kupongezana na
kuwashukuru walimu wao
Mkuu wa Shule Madam Lubasi na Makamu mkuu
wa shule wakikata keki kwa pamoja huku wahitimu
wakishuhudia zoezi hilo kwa umakini
Mhitimu akiikatakata keki katika vipande vidogovidogo
Picha zinazofuata ni baadhi ya walimu wakilishwa keki na wanafunzi wao
Picha zinazofuata Mkuu wa Shule akiwalisha keki wanafunzi wake
Kwa jinsi keki ilivyokuwa tamu
Mkuu wa Shule aliamua kujilisha keki mwenyewe
Mkuu wa Shule kwa niaba ya jumuia ya wana Mwanzi Sec. anawatakia wahitmu hawa kila la heri na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa Mwanzi Sec. popote waendapo.
Imeletwa kwenu na Mwalimu Furaha Venance
Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Masomo ya Kompyuta (ICS)
Anapatikana kwa namba 0715335558 / 0755440699
instagram: @fullraha17
HAYA NDIYO MATOKEO YAO YA KIDATO CHA SITA BAADA YA KUTANGAZWA
No comments:
Post a Comment