Thursday, January 17, 2013

YALIYOJITOKEZA KATIKA KIKAO CHA WAZAZI NA WALIMU WA MWANZI SEKONDARI

Leo tulikuwa na kikao cha wazazi wa kidato cha pili na walimu wa Mwanzi Sekondari, ni muda mrefu tumekuwa na kawaida ya kuwaita wazazi kuja shuleni kwa ajili ya kupewa taarifa mbalimbali za watoto wao lakini jambo la kusikitisha wamekuwa wakihudhuria wachache.
 
Mara baada ya matokeo ya kidato cha pili kutoka, tuliamua tuitishe kikao cha wazazi wa wanafunzi wa kidato cha pili ili kuzungumza nao, ajenda kubwa zilikuwa ni:
1. Kufungua kikao
2. Hali ya Taalumu
3. Hali ya Nidhamu
4. Ulipaji wa michango ya shule
5. Utoaji wa matokeo ya kidato cha pili kwa wazazi
6. Mengineyo
 
katika kikao hicho, kwa kuwa katika barua za wito kwa wazazi tuliandika kuwa waje kuchukua matokeo, wazazi wengi walihudhuria kiasi kwamba hata ukumbi tuliotumia kwa ajili ya kikao hicho ulikuwa mdogo.
 
jambo la kushukuru mungu wazazi wengi walituelewa kile tulichozungumzia na walionekana kuguswa sana na taarifa tulizokuwa tunawapa, kwa mfano katika hali ya taaluma tuliwaambia wazazi na ndo ukweli ulivyo, mtihani wa taifa kidato cha pili mwaka 2011 matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
 
   wanafunzi 154 walifanya mtihani huo
    wanafunzi 14 ndo walipata alama nzuri yaani walifaulu,
 
kwa maana hiyo kama wanafunzi hao mwaka huo wangetakiwa kurudia, ni wanafunzi 140 wangerudia darasa na wanafunzi 14 tu, ndiyo wangeendelea na masomo ya kidata cha tatu.
 
lakini kwa mwaka jana 2012 ambao matokeo yao ndiyo yametoka hivi karibu, shule ya sekondari tumeonekana kupiga hatua kubwa sana kwa mfano:
 
Wanafunzi waliofanya mtihani ni wanafunzi 178
wanafunzi waliofaulu ni wanafunzi 148 sawa na asilimia 84 [84%]
wanafunzi waliofeli ni wanafunzi 30 sawa na asilimia 16 [16%] na ndiyo wanaotakiwa kurudia kidato cha pili.
 
hivyo tukiangalia matokeo hayo ya mwaka 2011 na haya ya sasa utaona tu kuwa tumepiga hatua, tena sana. jambo la muhimu tuliwaomba hao wazazi watuunge mkono ili hawa watoto waje kutupa matokeo mazuri mara watakapomaliza kidato cha nne. wazazi wametuahidi kuwa watatuunga mkono.
 
Kiwilaya shule yetu imekuwa ya 20 kati ya shule 30, lakini kumbuka kuwa nafasi hii ni pamoja na zile shule ambazo zilikuwa na wanafunzi 07, 11, 30, 40 80 n.k kama tungekuwa tumelinganishwa na shule ambazo tuna idadi sawa ya wanafunzi, basi tungekuwa na nafasi nzuri, kumbukeni kuwa kufundisha darasa lenye idadi kubwa ya wanafunzi kama tuliokuwa nao sisi ni kazi kubwa sana.
 
Jambo la kushukuru Mungu na la kujivunia Wilaya yetu imejitahidi sana ukilinganisha na wilaya zingine, zipo wilaya zina shule ambazo wanafunzi wote wamefeli.
 
changamoto tuliyonayo ni wazazi kulipia michango na ada kwa watoto wao, nidhamu za wototo, utoro, ushirikiano mdogo kutoka kwa wazazi n.k
 
mambo mengine tuliyojadili ni hayo ya nidhamu, kuwahamasisha wazazi kulipia michango na ada kwa wakati na kufuatilia mienendo ya watoto wao huko nyumbani na huku shuleni, na vilevile tulitoa matokeo ya watoto wao. hapa wapo wazazi waliochekelea na wale walionuna au kuhuzunika.
 
kwa taarifa hii naomba niishie hapa, nakusanya data ambazo taziweka humu kuonesha wilaya yetu kwa shule zote, wamefanya mtihani wangapi, wangapi wamefaulu na wangapi wamefeli.
 
asanteni sana
 
TUKISHIRIKIANA KWA PAMOJA! TUTAIBADILISHA MANYONI
 
Taarifa hii imetolewa na Mwl. Venance F. ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho