Mwl. Ntiruka E.
Hatimaye shule ya secondari mwanzi imepata mkuu mpya anayejulikana kwa jina la Emanuel Ntiruka, mwalimu mkuu huyo mpya anayetoka shule ya secondari kizigo anachukua nafasi ya Ezra Shukia ambaye kwa mabadiliko hayo anaenda kuwa mkuu wa shule ya Rungwa. wakuu hao wametakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vipya kuanzia jumatatu ya tarehe 11/03/2013 na tayari ndugu Ntiruka amesharipoti Mwanzi siku ya jana. mabadiliko hayo yametokea baada ya tetesi za muda mrefu za kubadilishiwa vituo baadhi ya walimu wakuu lengo likiwa ni kuongeza ufanisi.
Haya ni mabadiliko ya pili makubwa kutokea baada ya yale ya manyoni sekondari. ambapo mkuu wa shule hiyo ndugu Shalua kupelekwa mwanzi kuwa mwalimu wa kawaida na mama Lema aliyekuwa mkuu wa kamenyanga kuchukua nafasi hiyo. Habari za kuhamishwa kwa Shukia zilianza kusambaa ijumaa jioni wapo waliona habari hzo ni kama uzushi vile na wengine waliziamini.
Shukia J.E
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mabadiliko hayo si kuwa yameikumba Mwanzi tu kama wengi wanavyodhani.
Hadi tunawaletea taarifa hizi hatujaweza kupata majina ya shule zingine na wakuu wake ambao wamekumbwa na mabadiliko hayo.
Ikumbukwe kuwa ndugu, Ntiruka kabla ya kwenda Kizigo alikuwa mwalimu wa Mwanzi kuanzia 2008, na 2009 aliteuliwa kukaimu nafasi ya Mkuu wa Shule hiyo baada ya aliyekuwa mkuu shuleni hapo mwl. Mjungu kustaafu. 2010 Ntiruka akapelekwa kizigo kuwa Mkuu wa shule hiyo akimkabidhi Shukia shule na sasa anarudi Mwanzi Shukia kumkabidhi Ntiruka Mwanzi.