Thursday, September 26, 2013


HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI

SHULE YA SEKONDARI MWANZI

 

TANGAZO LA KIKAO CHA WAZAZI

 
Shule ya Sekondari Mwanzi inapenda kuwatangazia wazazi wote wenye watoto wao wanaosoma Shule ya Sekondari Mwanzi kuwa, siku ya jumanne tarehe 01/10/2013 kutakuwa na kikao cha wazazi na wafanya kazi wa shule hii kwa ajili ya kujadili maendeleo ya shule na wanafunzi wa Mwanzi.


Hivyo wazazi wote wenye watoto katika shule hii, mnaombwa kuhudhuria bila kukosa, tushirikiane kwa pamoja namna ya kuinua taaluma ya shule yetu na watoto wetu.

 
Ukiliona tangazo hili, wajulishe na wenzako

Limetolewa na,

…………………………….

E. Ntiruka

MKUU WA SHULE

Wednesday, September 4, 2013

WALIMU WA MWANZI WAAGA WAFANYAKAZI WENZAO, AMBAO WAMEHAMA

 
Na. Mwl. Venance F.
 
Jana Tarehe 03/09/2013, walimu wa Mwanzi, wamefanya Sherehe fupi kuwaaga walimu wa mazoezi pamoja na walimu na wafanyakazi wasiowalimu, ambao wamehamia sehemu mbalimbali, walimu waliogwa ni pamoja na Mwl. Nyakigha, aliyekuwa Mwalimu wa Nidhamu, ambaye amehamia Musoma kuwa Afisa Takwimu na Vielelezo [Sekondari], Mwalimu Shukia aliyekuwa Mkuu wa Shule, ambaye amehamia Singida shule ya Sekondari Mwenge, Fundi Jimmy Mhamiji aliyeamia Tabora Boys, na Muhasibu Philipo S. aliyeamia Dodoma, Manispaa, zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo la kuwaaga wenzetu:
 
 
Kutoka kushoto, Mkuu wa Shule, Ntiruka, akiwa na
waagwa,Jimmy Mhamiji na Mwl.Nyakigha
 
Mkuu wa Shule akitoa neno
 
Fundi Jimmy naye akitoa neno
 
Mwalimu Nyakigha naye akitoa yake ya moyoni
 
 Unamjua huyu! ndiyo Dj. Lubasi
 
Aliyemwakilisha Mkuu wa Shule aliyehama, ndugu Shukia
 
Hapa inaelekea mambo yalikuwa safi, huyo ndo white mwenyewe,
 mwalimu Luka ambaye alikuwa mwenyekiti wa sherehe.
 
Muda wa zawadi huo!!!!!!
 
Walimu hao wakipeleka zawadi
 
Makamu mkuu, akimkabidhi zawadi Fundi Jimmy
 
Mwalimu Deborah akimkabidhi zawadi mwalimu Nyakigha
ambaye amehamia Musoma
 
Hapo mi sitii neno
 
Mwl, Jane Mwaigonela, akikabidhi zawadi kwa
mkuu wa shule, ambayo aliipokea kwa niaba ya Mhasibu,
Philipo ambaye amehamia Dodoma manispaa
 
Prosper na zawadi walimu wenzake wakimsindikiza
 
 
    Mwalimu Prosper akimkabidhi zawadi, Bwana Inno
ambaye alikuwa akimwakilisha Shukia, ambaye
amehamia Mwenge Sec.
 
JUMUIYA YA WANA MWANZI
INAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA KULITUMIKIA TAIFA HUKO MUENDAKO
 
Imeandaliwa na Mwl. Venance.