Thursday, December 1, 2016

MWANZI DAY: PICHA ZAIDI YA 40 ZA TUKIO ZIMA HIZI HAPA

Na. Mwl. Venance
Tarehe 30/11/2016 ilikuwa siku maalumu kwa walimu wa Shule ya Sekondari Mwanzi. Walimu walifunga mwaka wa masomo 2016 kwa kushiriki michezo mbalimbali. Siku hiyo maalumu ilipewa jina la Mwanzi Day. picha za tukio hilo hizi hapa:



  Walimu wakijadiliana jambo kabla ya kuelekea uwanjani



 Kwaito ilichezwa kama kawaida

 Mwl. Moris akifanya mazoezi ya kukimbia na gunia
 kabla ya kushiriki mchezo huo

 Walimu katika pozi



 Mwl. Venance akifanya yake kama Mc akisaidiana na 
Mwl Moris (aliyekaa juu ya meza)

 Mkuu wa Shule akimpongeza Mwl. Mwabeza 
kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mchezo wa kukuna nazi

 Mwl. Venance katika mchezo wa kukuna nazi


 Mwl. Mwabeza katika Mchezo wa kukuna nazi

 Mwl. Mwaigonela akipongezwa na Mkuu wa Shule
 kwa kuwa mshindi wa kwanza mbio za mita 100 wanawake

 Mwl. Venance (kushoto) na Mwl. Mwabeza 
wakishiriki mchezo wa kukuna nazi



 Mzee wa mikwara, Mwl. Manyasa akionesha manjonjo yake


Mwl. Mandia na wanafunzi wa kidato cha kwanza



Walimu katika pozi


Mwl. Maghway akionesha mfano jinsi ya kushiriki zoezi la kukuna nazi

Mwl. Ginatio akionesha mfano jinsi ya kushiriki zoezi la kukuna nazi

 Mkuu wa Shule pamoja na walimu wake wakifuatilia 
michezo inayoendelea kwa umakini


 Walimu wakijadiliana jambo kabla ya kushiriki mchezo wa kuvuta kamba

Mwl. Madata akipongezwa na Mkuu wa shule 
kwa kuwa mshindi katika mchezo wa mbio 
za kujaza mchanga katika chupa

 
Mwl. Mandia akipongezwa na Mkuu wa Shule kwa kuwa 
mshindi wa kwanza kurusha tufe

 Mkuu wa Shule akimpongeza Mwl. Japhet kwa kuwa 
mshindi wa mbio za kujaza mchanga kwenye chupa


 Mkuu wa Shule, Madam Lubasi akimpongeze Mwl. Yobele
kwa kuwa mshindi wa kwanza wa kutembea na yai kwa kijiko mdomoni

  Mwl. Yobele akishiriki katika mchezo wa kurusha tufe

  Mwl. Mandia akishiriki katika mchezo wa kurusha tufe

 Mwl. Moris akishiriki katika mchezo wa kurusha tufe

 Mwl. Sylvery akirusha tufe



 Walimu wakishiriki mchezo wa Rede

Mkuu wa Shule akimpongeza Mwl. Mandia 
kwa kuwa mshindi katika mchezo wa rede

Saturday, August 6, 2016

HABARI PICHA: MKUU WA WILAYA YA MANYONI AIKABIDHI SHULE YA SEKONDARI MWANZI MADAWATI. AAHIDI NEEMA TENA


Na Mwl. Furaha Venance
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Manyoni, kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mkuu wa wilaya amesema kuwa kiasi cha Tsh milioni 15 ambazo amechangiwa na waliokuwa wafanyakazi wenzake wizara ya Mambo ya Nje zitatumika kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari. alisema kuwa kiasi hicho cha pesa kitagawanya katika halmashauri mbili, ya Manyoni na ile ya Itigi.
"...Ingawa Itigi wamemaliza tatizo la madawati, kiasi cha pesa hizi zitatengwa kulipia madeni katika halmashauri hiyo..maana wana madeni bado" amesema mkuu huyo wa wilya.

Aidha aliwaomba madiwani wa Halmashauri ya Manyoni kuitisha harambee ili Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ukae vizuri. alitumia pia nafasi hiyo kuishukuru mamlaka ya Bandari kwa kuchangia madawati hayo.

Awali Afisa Taluuma wa Halmashauri ya Manyoni, Bw. Jamhuri Kidumu alisema kuwa madawati hayo yametengezwa kwa msaada wa Mamlaka ya Bandari ambao walichangia kiasi cha tsh milioni 10. Madawati 109 yamegawanywa shule za msingi na meza 70 na viti 70 shule za sekondari.

Kuhusu upungufu wa madawati katika shule, Afisa taaluma huyo alisema kuwa, shule zilizoko pembezeni ya mji hazina matatizo makubwa ya madawati kutokana na uchache wa wanafunzi katika shule hizo. Tatizo liko katika shule zilizoko mjini ambazo zina idadi kubwa ya wanafunzi.

Mkuu wa shule ya Mwanzi alitoa taarifa kuwa shule yake ina upungufu wa meza na viti 115 mpaka sasa. Meza na viti walivyopewa itasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo katika shule yake.

Matukio katika Picha tazama hapa chini



 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni akizungumza na wananchi

 Baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Manyoni 
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya



Wanafunzi wa Mwanzi Sekondari na walimu wao 
wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya

  Mkuu wa Wilaya (kulia) akizungumza na Afisa Taaluma wilaya



 Mkuu wa Wilaya akizungumza na wanafunzi wa Mwanzi Sekondari


 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya Mh. Mwambe, Mbunge wa Manyoni Mashariki,
 Mh.Mtuka na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni, Mh. 

Wanafunzi wa Mwanzi Sekondari wakiwa wamekalia madawati hayo.