Saturday, August 6, 2016

HABARI PICHA: MKUU WA WILAYA YA MANYONI AIKABIDHI SHULE YA SEKONDARI MWANZI MADAWATI. AAHIDI NEEMA TENA


Na Mwl. Furaha Venance
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Manyoni, kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mkuu wa wilaya amesema kuwa kiasi cha Tsh milioni 15 ambazo amechangiwa na waliokuwa wafanyakazi wenzake wizara ya Mambo ya Nje zitatumika kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari. alisema kuwa kiasi hicho cha pesa kitagawanya katika halmashauri mbili, ya Manyoni na ile ya Itigi.
"...Ingawa Itigi wamemaliza tatizo la madawati, kiasi cha pesa hizi zitatengwa kulipia madeni katika halmashauri hiyo..maana wana madeni bado" amesema mkuu huyo wa wilya.

Aidha aliwaomba madiwani wa Halmashauri ya Manyoni kuitisha harambee ili Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ukae vizuri. alitumia pia nafasi hiyo kuishukuru mamlaka ya Bandari kwa kuchangia madawati hayo.

Awali Afisa Taluuma wa Halmashauri ya Manyoni, Bw. Jamhuri Kidumu alisema kuwa madawati hayo yametengezwa kwa msaada wa Mamlaka ya Bandari ambao walichangia kiasi cha tsh milioni 10. Madawati 109 yamegawanywa shule za msingi na meza 70 na viti 70 shule za sekondari.

Kuhusu upungufu wa madawati katika shule, Afisa taaluma huyo alisema kuwa, shule zilizoko pembezeni ya mji hazina matatizo makubwa ya madawati kutokana na uchache wa wanafunzi katika shule hizo. Tatizo liko katika shule zilizoko mjini ambazo zina idadi kubwa ya wanafunzi.

Mkuu wa shule ya Mwanzi alitoa taarifa kuwa shule yake ina upungufu wa meza na viti 115 mpaka sasa. Meza na viti walivyopewa itasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo katika shule yake.

Matukio katika Picha tazama hapa chini



 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni akizungumza na wananchi

 Baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Manyoni 
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya



Wanafunzi wa Mwanzi Sekondari na walimu wao 
wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya

  Mkuu wa Wilaya (kulia) akizungumza na Afisa Taaluma wilaya



 Mkuu wa Wilaya akizungumza na wanafunzi wa Mwanzi Sekondari


 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya Mh. Mwambe, Mbunge wa Manyoni Mashariki,
 Mh.Mtuka na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni, Mh. 

Wanafunzi wa Mwanzi Sekondari wakiwa wamekalia madawati hayo.