Tuesday, May 9, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: WAHITIMU WA KIDATO CHA VI 2017 MWANZI SEC. WAWAAGA WALIMU WAO KIAINA

Na. Mwl. Venance F.
Wanafunzi wa kidato cha sita 2017 mara baada ya kumaliza mtihani wao wa mwisho leo (Jumanne, tar. 9/5/2017) waliamua kuwashukuru na kuwaaga walimu wao. Walimu walitoa nasaha mbalimbali kwa wahitimu hao zoezi lilioenda sambamba na wanafunzi kuwalisha keki walimu wao kama ishara ya shukrani lakini pia Mkuu wa shule kwa niaba ya walimu wote aliwalisha keki wahitimu hao kama ishara ya kuwatakia mema na kukubari shukrani yao. Nimekuwekea hapa picha zinazoeleza tukio zima:

 Wanafunzi wa Kidato cha Sita 2017 wakiwa wamekusanyika
 katika ofisi ya Mkuu wa Shule kusikiliza nasaha za mwisho
 kabla ya kutawanyika kuelekea mtaani

 Afande nae akaamua kutwanga foto na wanafunzi
 alioshiriki kuwasimamia


 Mkuu wa Shule Madam, Lubasi pamoja na afande Lucy 
wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi




 Mkuu wa Shule akiwa katika picha ya pamoja
 na baadhi ya wahitimu kidato cha VI 2017 

 Wahitimu waliandaa keki kwa ajili ya kupongezana na 
kuwashukuru walimu wao


 Mkuu wa Shule Madam Lubasi na Makamu mkuu
 wa shule wakikata keki kwa pamoja huku wahitimu 
wakishuhudia zoezi hilo kwa umakini

Mhitimu akiikatakata keki katika vipande vidogovidogo

Picha zinazofuata ni baadhi ya walimu wakilishwa keki na wanafunzi wao








Picha zinazofuata Mkuu wa Shule akiwalisha keki wanafunzi wake





Kwa jinsi keki ilivyokuwa tamu 
Mkuu wa Shule aliamua kujilisha keki mwenyewe


Mkuu wa Shule kwa niaba ya jumuia ya wana Mwanzi Sec. anawatakia wahitmu hawa kila la heri na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa Mwanzi Sec. popote waendapo.
Imeletwa kwenu na Mwalimu Furaha Venance
Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Masomo ya Kompyuta (ICS)
Anapatikana kwa namba 0715335558 / 0755440699 
instagram: @fullraha17
HAYA NDIYO MATOKEO YAO YA KIDATO CHA SITA BAADA YA KUTANGAZWA