Tuesday, June 27, 2017

HABARI NA PICHA: MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BWENI LA WASICHANA MWANZI SEKONDARI

Na. Mwl. Venance, F. 

Mwenge wa Uhuru leo tarehe 27/06/2017 umetua katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni. Katika moja ya miradi iliyozinduliwa na kuwekea jiwe la msingi katika halmashauri hii ni pamoja na Ujenzi wa Bweni la Wasichana shuleni hapa. Mkuu wa shule Mama Janeth Lubasi akisoma taarifa fupi mbele ya Kiongozi wa mbia za mwenge Bw. Amour Hamad Amour, alisema kuwa, ujenzi wa bweni hilo ulianza tangu mwaka 2010. Uendelezaji wake uliendelea baada ya kuungua kwa bweni la wasichana shuleni hapo. Aidha Mkuu huyo wa Shule aliongeza  kuwa, mradi huo unajengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, ikiwemo Halmashauri ya Manyoni, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wafanyabiashara wa Manyoni pamoja na nguvu za wananchi wa Manyoni. Mkuu wa Shule alisema kuwa mradi  ukikamilika utaweza kubeba jumla ya wanafunzi 50 kwa wakati mmoja.  

Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Amour Hamad Amour mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi husika. Alimpongeza Mkuu wa Shule, Mkandarasi na wadau wote waliofanikisha mradi huu tena kwa kiwango bora.  Akimuelekea Mkuu wa Shule, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema, "Hongera sana mama...yaani hapa umepata Hosteli. Mimi nimeukubali kwa asilimia mia." aidha alimtaka mkuu huyo wa shule kuwahimiza wanafunzi wasome kwa bidii, wafundishwe uzalendo na kuijua nchi yao.

Hapa chini nimekuwekea picha za tukio zima..... 

Mkuu wa Shule akisoma taarifa ya mradi
 Mkuu wa Shule akiusubiri Mwenge wa Uhuru

Burudani za ngoma za asili zilikuwepo

Wazee wa matarumbeta pia walikuwepo kutumbuiza

 Bweni la wasichana linalojengwa




 



















Habari na picha na Mwl. Venance, F.
0715 33 55 58/0755 44 06 99