Thursday, July 18, 2019

HABARI PICHA: WALIMU WA MWANZI WAPONGEZWA KWA MATOKEO MAZURI KIDATO CHA SITA 2019

Na. Mwl. Venance, F.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwanzi kwa kushirikiana na Bodi ya shule, wamewapongeza walimu wao kwa kazi nzuri na kufanikisha shule kuwa na matokeo mazuri ya kidato cha sita 2019 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani hivi karibuni.

Pamoja na pongezi hizo walizomiminiwa walimu kutoka kwa Mkuu wao na wajumbe wa bodi, waliandaliwa chakula cha mchana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi, Mzee Msongo aliwataka walimu waendelee kujituma zaidi na kuhakikisha shule inapata matokeo mazuri zaidi kwa wanafunzi wa kidato cha NNE wanaotarajiwa kufanya mitihani yao ya taifa mwaka huu.

 Mkuu wa Shule, Janeth Lubasi akizungumza na 
walimu pamoja na wajumbe wa Bodi

 Walimu wakiombea chakula

Hapo ni kama Mkuu anamwambia Mwl. Abdul kwenye simu "Aisee sijakuona leo...Kuku wako anakula James huku!!!"

 Mkuu wa shule mwenye kikoi cheusi akiwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi. Mwenyeki wa bodi nikama anamwambia Mkuu "Aisee ungeniambia mapema kama kuna kuku wa aina hii nisingekula nyumbani..."

 Makamu Mkuu wa Shule hapo ni kama anasema "Ongeza na paja hilo" (kwa lafudhi ya kikurya)

 Mkuu wa Shule na baadhi ya wajumbe wa Bodi


 Baadhi ya Walimu

  Baadhi ya Walimu

 Baadhi ya Walimu. Mwl Epimack ni kama anamwambia mwl Roby.."Madam huyu kuku mtamuuuuu".

  Baadhi ya Walimu, Makamu Mkuu wa shule ni kama anasema "Mbona Joshua kama anaenda kupiga paper two!"

Mwalimu Amath kama anasema "Huyu kuku au mbuzi?"

 Baadhi ya Walimu... Mwl Mgode ni kama anajiuliza.."Nianze na wali au kuku!!! Aaah! ngoja nianze na Kuku kwanza nisije nikashiba wali kuku akanishinda"

Mkuu wa shule akizungumza...Hapa ni kama anasema "Jamani hawa kuku mnawaonaje..mi mwenzenu nimeshindwa hata kunywa soda tainywa nyumbani"

Mwenyekiti wa Bodi akizungumza na walimu Hapa ni kama anasema..."Tangu nipige marufuku bodaboda naona matokeo yanazidi kuwa mazuri. Si mnaona hadi wasichana wamepata ONE?"

(Maelezo yaliyowekwa kwenye fungua semi na funga semi ni utani tu wa mwandishi hayahusiani na wahusika.)



Imeandaliwa na Mwl. Venance, F.
Mkuu wa idara ya ICS
0755440699

Wednesday, July 17, 2019

MAKAMU MKUU WA MWANZI SEKONDARI ATEULIWA KUWA MKUU WA SHULE YA ITIGI SEKONDARI

SECOND MASTER
Na. Mwl.Venance, F.
Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwanzi, Jacob Mwabeza (pichani) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Itigi iliyopo katika Halmashauri ya Itigi Mkoani Singida. Uteuzi huo umefanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Mkuu wa shule hiyo, Ndugu, Kansheba kuteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo Singida Mjini.

Mkuu wa shule amemteua Mwl. Sylvery Rashid kuwa Makamu Mkuu wa Shule kuziba nafasi hiyo.

Mkuu wa Shule ya Mwanzi, pamoja na jumuiya ya Mwanzi Sekondari wanampongeza na kumtakia kila la heri Mwl. Mwabeza katika majukumu yake hayo mapya. 


Wednesday, June 12, 2019

JOINING INSTRUCTIONS KIDATO CHA V 2019 MWANZI SEC. HII HAPA


HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI
SHULE YA SEKONDARI MWANZI
 Shule ya Sekondari Mwanzi iko umbali wa Kilometa moja na nusu (1.5 km) Kaskazini Mashariki mwa halmashauri ya  Wilaya ya Manyoni.Muhula wa masomo unaanza tarehe 08/07/2019.  Hivyo Mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni tarehe
06/07/2019 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 22/07/2019.
 Ingia katika link hapa chini kupata fomu ya maelekezo:

JOINING INSTRUCTIONS KIDATO CHA V 2019 MWANZI SEC BOFYA HAPA