Saturday, August 16, 2014

MWANZI YALALA YAKANDAMIZWA 3:1 NA KILIMATINDE, SASA KUWASUBIRI ITIGI SEC.


Na. Mwl. Venance F.
Timu ya mpira wa miguu ya shule ya sekondari Mwanzi imeshindwa kufua dafu mbele wenzao wa Kilimatinde katika mtanange uliopigwa jana ijumaa katika shule ya sekondari Kilimatinde. Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa shule ya sekondari kilimatinde ilikuwa mbele kwa mabao 3:1
Mchezo huo ulianza  saa 11:00 jioni kwa kuchezwa dakika 30 kwa kila kipindi, hadi timu hizo zinakwenda mapumziko mabao yalikuwa ni 1:1
Mambo yalikuja geuka kipindi cha pili kwa timu ya mwanzi kuongezwa mabao mengine mawili na hivyo kuhitimisha mtanange huo kwa Kilimatinde kuibuka washindi kwa 3:1.

walimu kama wanafunzi wao

Katika hali isiyotarajiwa timu ya walimu wa Mwanzi nao walitandikwa mabao kama waliyotandikwa wanafunzi wao. Mchezo huo kati ya walimu wa Mwanzi Sec. Na wenzao wa Kilimatinde ndiyo ulikuwa mchezo wa kwanza kuanza kabla ya ule wa wanafunzi, hadi mpira unaisha walimu wa Mwanzi walilala kwa mabao 3:0.

wasichana Mwanzi wajitutumua 

Timu ya netball iliwafuta machozi Mwanzi Sec kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 12 kwa 11, mchezo huo uliokuwa wakuvutia kila pande zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu, lakini mpaka mpira unaisha Mwanzi Sec. Waliibuka washindi kwa vikapu 12:11.
Kilimatinde wadaiwa kuchezesha mamluki
Katika hali isiyotarajiwa timu ya walimu wa Kilimatinde ilionekana kuchezesha wachezaji mamluki, madai haya yaliibuka baada kuonekana mchezaji mmoja wa timu hiyo kuonekana amenyoa mtindo wa kiduku, na kama inavyofahamika kwa maadili ya kazi mwalimu hawezi kunyoa nywele zake kwa mtindo huo, hata hivyo kulikuwa na madai mengine kuwa kilimatinde ilicheza walimu wengine kutoka shule ya Sekondari St. John na hivyo walimu wa Mwanzi kujigamba kuwa walicheza na shule mbili.
MATUKIO KATIKA PICHA
                                                    Kikosi cha walimu wa Mwanzi Sec.

                                              Kutoka kushoto Mwl. Varelian wa Kilimatinde na
 Mwl. Venance wa Mwanzi Sec. 

                                          Mwl. Emanuel {Second Master} akitoa maelekezo
 kwa walimu wake

                                       Walimu wakipambana uwanjani, mwenye jezi nyekundu
 namba 10 ni mwalimu wa Kilimatinde aliyezua sokomoko
kuwa ni mamluki cheki kiduku hicho ndicho kilichozua utata

                                          Mkuu wa Shule ya Mwanzi, Lubasi J. akitoa
                         maelekezo pembeni yake kulia ni mwl. Melesi {Second Master K/tinde}

                                             Kikosi cha wanafunzi mwanzi sec wakipiga dua
                                                                    Wakipiga tizi
                                     Refa alikuwa mwalimu Moris hapo akiwapa maelekezo
                           kikosi cha Mwanzi wenye njano, waliovalia nyekundu ni wa Kilimatinde

                                                   kikosi cha wasichana Mwanzi Sec

kikosi cha mwanzi sec wanafunzi

 Habari na picha na mwalimu Venance F.

Thursday, August 14, 2014

MWANZI SEC. KUUMANA NA KILIMATINDE KESHO IJUMAA

Na. Mwl. Venance F.
Moja ya kikosi hatari cha mwanzi kilichocheza
 na Chikuyu Sec. miaka ya nyuma

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwanzi kufanya ziara ya kitaaluma na michezo katika shule ya sekondari Kilimatinde, katika Ziara hiyo michezo mbalimbali itachezwa. Mwalimu wa Michezo wa Mwanzi Sekondari, Mwl Mwaigonela akitoa ratiba ya ziara hiyo kwa www.mwanzisec.blogspot.com alisema kuwa kabla ya mechi hizo kucheza kutatanguliwa na mdahalo kati ya wanafunzi wa shule hizo, itafuatiwa na mechi kati ya walimu wa Mwanzi Sec. na walimu wa Kilimatinde Sec. na baadaye kuhitimishwa na mechi za wanafunzi.

Akielezea maandalizi ya ziara hiyo, mwalimu huyo alisema kuwa, taratibu zote zimewekwa sawa, wanafunzi wa Mwanzi wana hali ya kuibuka washindi katika michezo yote iliyopangwa kufanyika, huku walimu nao wakiahidi kuwafundisha soka walimu wenzao wa Kilimatinde.

Mwalimu wa Zamu, Mwalimu Sylvery Hussein akiwatangazia wanafunzi wake aliwataka wakajiandae na safari ya kesho, na pia wasisahau kubeba vifaa vya michezo bila kusahau sahani za chakula chakula kitatolewa huko huko kwa wanafunzi wote ili kuhakikisha Kilimatinde wanapewa dozi za maana.

Mungu ibariki Mwanzi Sec.