Na. Mwl. Venance, F.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Amour Hamad Amour mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi husika. Alimpongeza Mkuu wa Shule, Mkandarasi na wadau wote waliofanikisha mradi huu tena kwa kiwango bora. Akimuelekea Mkuu wa Shule, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema, "Hongera sana mama...yaani hapa umepata Hosteli. Mimi nimeukubali kwa asilimia mia." aidha alimtaka mkuu huyo wa shule kuwahimiza wanafunzi wasome kwa bidii, wafundishwe uzalendo na kuijua nchi yao.
Hapa chini nimekuwekea picha za tukio zima.....
Mkuu wa Shule akisoma taarifa ya mradi
Mkuu wa Shule akiusubiri Mwenge wa Uhuru
Burudani za ngoma za asili zilikuwepo
Wazee wa matarumbeta pia walikuwepo kutumbuiza
Bweni la wasichana linalojengwa
Habari na picha na Mwl. Venance, F.
0715 33 55 58/0755 44 06 99

























