Thursday, September 26, 2013


HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI

SHULE YA SEKONDARI MWANZI

 

TANGAZO LA KIKAO CHA WAZAZI

 
Shule ya Sekondari Mwanzi inapenda kuwatangazia wazazi wote wenye watoto wao wanaosoma Shule ya Sekondari Mwanzi kuwa, siku ya jumanne tarehe 01/10/2013 kutakuwa na kikao cha wazazi na wafanya kazi wa shule hii kwa ajili ya kujadili maendeleo ya shule na wanafunzi wa Mwanzi.


Hivyo wazazi wote wenye watoto katika shule hii, mnaombwa kuhudhuria bila kukosa, tushirikiane kwa pamoja namna ya kuinua taaluma ya shule yetu na watoto wetu.

 
Ukiliona tangazo hili, wajulishe na wenzako

Limetolewa na,

…………………………….

E. Ntiruka

MKUU WA SHULE

Wednesday, September 4, 2013

WALIMU WA MWANZI WAAGA WAFANYAKAZI WENZAO, AMBAO WAMEHAMA

 
Na. Mwl. Venance F.
 
Jana Tarehe 03/09/2013, walimu wa Mwanzi, wamefanya Sherehe fupi kuwaaga walimu wa mazoezi pamoja na walimu na wafanyakazi wasiowalimu, ambao wamehamia sehemu mbalimbali, walimu waliogwa ni pamoja na Mwl. Nyakigha, aliyekuwa Mwalimu wa Nidhamu, ambaye amehamia Musoma kuwa Afisa Takwimu na Vielelezo [Sekondari], Mwalimu Shukia aliyekuwa Mkuu wa Shule, ambaye amehamia Singida shule ya Sekondari Mwenge, Fundi Jimmy Mhamiji aliyeamia Tabora Boys, na Muhasibu Philipo S. aliyeamia Dodoma, Manispaa, zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo la kuwaaga wenzetu:
 
 
Kutoka kushoto, Mkuu wa Shule, Ntiruka, akiwa na
waagwa,Jimmy Mhamiji na Mwl.Nyakigha
 
Mkuu wa Shule akitoa neno
 
Fundi Jimmy naye akitoa neno
 
Mwalimu Nyakigha naye akitoa yake ya moyoni
 
 Unamjua huyu! ndiyo Dj. Lubasi
 
Aliyemwakilisha Mkuu wa Shule aliyehama, ndugu Shukia
 
Hapa inaelekea mambo yalikuwa safi, huyo ndo white mwenyewe,
 mwalimu Luka ambaye alikuwa mwenyekiti wa sherehe.
 
Muda wa zawadi huo!!!!!!
 
Walimu hao wakipeleka zawadi
 
Makamu mkuu, akimkabidhi zawadi Fundi Jimmy
 
Mwalimu Deborah akimkabidhi zawadi mwalimu Nyakigha
ambaye amehamia Musoma
 
Hapo mi sitii neno
 
Mwl, Jane Mwaigonela, akikabidhi zawadi kwa
mkuu wa shule, ambayo aliipokea kwa niaba ya Mhasibu,
Philipo ambaye amehamia Dodoma manispaa
 
Prosper na zawadi walimu wenzake wakimsindikiza
 
 
    Mwalimu Prosper akimkabidhi zawadi, Bwana Inno
ambaye alikuwa akimwakilisha Shukia, ambaye
amehamia Mwenge Sec.
 
JUMUIYA YA WANA MWANZI
INAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA KULITUMIKIA TAIFA HUKO MUENDAKO
 
Imeandaliwa na Mwl. Venance.

Friday, July 12, 2013

MWANZI SEKONDARI

 

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
 
 
WANAFUNZI WA MWANZI WALIOCHAGULIWA
KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO SHULE MBALIMBALI
 
Hawa ni wanafunzi waliomaliza Mwanzi Sec. na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano:
  NOEXAM NOJINA LA MWANAFUNZISHULE AENDAYOMASOMO
1S0662/0086 Elibarick Clement Mwakaleli HGK
2S0662/0103 Isack Noah Moshi TechCBG
3S0662/0130 Paschali Makali LwangwaPCM
4S0662/0134 Peter Julius BinzaCBG
5S0662/0150 Stephano Christian Mwanzi PCM
6S0662/0154 Thomas Daniel BihawanaCBG
7S0662/0156 Tumaini Petro Itigi HGL
8S0662/0027 Limi Mshamindi Bwiru Girls CBG
9S0662/0034 Maria Simon Kondoa Girls HGK
10S0662/0042 Ocley Thadey Maswa Girls PCM
11S0662/0054 Rose Shedrack Maswa Girls PCM
TUNAWATAKIA KILA LA HERI WANAFUNZI WOTE
WALIOPATA NAFASI YA KUENDELEA NA MASOMO YA KIDATO CHA TANO

Sunday, June 30, 2013

ORODHA YA SHULE ZA SEKONDARI 1,200 ZITAKAZOFANYIWA UKARABATI

 
ORODHA YA SHULE ZA SEKONDARI 1,200 ZITAKAZOFANYIWA UKARABATI
 
        Katika hotuba hiyo tumechukua shule za Sekondari Manyoni tu.

NA.  JINA LA SHULE       WILAYA       MKOA
 
1043  ITIGI SEKONDARI    Manyoni         Singida

1044  CHIKUYU                    Manyoni        Singida
 
1045  MLEWA                        Manyoni       Singida
 
1046  MANYONI                    Manyoni       Singida

                                         1047  NKONKO                      Manyoni        Singida
  
 
WILAYA 15 AMBAKO ZITAJENGWA VYUO VYA UFUNDI STADI
AWAMU YA PILI
Na.  WILAYA     MKOA
 
     1.     Magu             Mwanza
2.     Serengeti        Mara
3.     Rorya             Mara
   4.     Kongwa         Dodoma
5.     Manyoni        Singida
  6.     Babati            Manyara
   7.     Hanang          Manyara
 
8.     Mkuranga      Pwani
9.     Kyela            Mbeya
10.   Sumbawanga  Rukwa
11.   Nkasi              Rukwa
12.   Nanyumbu      Mtwara
  13.   Tandahimba    Mtwara
14.   Liwale             Lindi
15.   Ruangwa         Lindi
 




 

 
 
 




 


Friday, May 31, 2013

Haya ndiyo matokeo ya kidato cha sita 2013 kwa shule mbili za A- LEVEL katika wilaya yetu ya Manyoni, na nafasi za shule hizo kimkoa na kitaifa.

MWANZI : DIV: I=0, II=14, III=24, IV=0, 0=0 Kimkoa, imeshika nafasi ya 2 kati ya shule 6
                                                                            Kitaifa imeshika nafasi 53 kati ya shule 329

ITIGI: DIV: I=0, II=6, III=45, IV=0, 0=0             Kimkoa, imeshika nafasi ya 4 kati ya shule 6
                                                                            Kitaifa imeshika nafasi 100 kati ya shule 329

Ukitaka kuingia moja kwa moja kuona matokeo ya shule hizo bofya hapa


ITIGI SEC:  http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/ACSEE_2013/s1032.htm