Wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Mwanzi wameamua kuisaidia jamii kwa kuamua kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye mahitaji ya kuongezewa damu katika hospitali mbalimbali mkoani Singida. Zoezi hilo la uchangiaji damu limefanyika jana jumanne tarehe 12/02/2013 katika Shule ya sekondari Mwanzi.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la uchangiaji damu.
Wanafunzi wa Mwanzi wakihamasishwa kuchangia damu
Mwanafunzi wa kidato cha nne akiangaliwa kama damu yake iko ya kutosha
Mwanafunzi wa kidato cha nne akiwa tayari kuchangia damu
kama anavyoonekana
Mwl. Deborah Mkombozi Akiulizwa maswali ya hapa na pale huku
mwalimu Lubasi pembeni kwa mbali akisubiri zamu yake ifike
Wanafunzi wakiwa tayari wameshatoa damu zao
Mwalimu Lubasi akipata vipimo kuangalia mapigo ya moyo n.k
Chumba kilichotumika ndo hiki, huku wengine wakijipoza na soda, biskuti
Haya sasa! chezea sindano wewe! Mwalimu Lubasi naye alijitolea damu
Inapendeza sana pale mwalimu Lubasi pembeni mwanafunzi wake
Kazi ya kuendelea kuhamasisha wengine kujitolea damu iliendelea
kufanyika katika bwalo la wanafunzi
Damu ambazo zilikuwa tayari zikiwekwa vizuri
Mwalimu Venance [Mwenye suti] naye alikuwepo
kuhakisha mambo yanaenda sawa
Mwalimu Moris, Venance, Jenipher na Nyakigha wakihakisha
hakuna mwanafunzi anayezagaa nje wakati wengine wakiwa
katika zoezi la kuchangiadamu
MUNGU AWABARIKI SANA
Picha na Habari imeandaliwa na Mwalimu Venance F.
No comments:
Post a Comment