Mwl. Venance F.
Leo katika Shule yetu ya Mwanzi, tulikuwa na kikao na wazazi wa watoto wanaosoma shule hii, lengo lilikuwa kukajadili maendeleo ya watoto wao, ya kitaaluma, nidhamu, utotoro na mengineyo, miongoni mwa waliohudhuria ukiachana na walimu wa Mwanzi, ni pamoja na Afisa Elimu Sekondari, Katibu CCM wilaya, Mratibu Elimu kata, Afisa Tarafa, Afisa Mtendaji Kata, Mwenyekiti wa bodi, na mjumbe wa bodi, wazazi waliazimia mambo mengi, miongoni mwa maazimio yalikuwa ni, wazazi kuchangia chakula ili watoto wao wawe wanapata chakula hapa shuleni, wazazi kuchangia ujenzi wa bweni [kumalizia bweni lililopo ambalo limefikia kwenye linta] na uzio wa shule, [hili ni mpango wa muda mrefu], kuchangia ujenzi wa maabara chumba kimoja, pia watoto wanaokabiliwa na mitihani ya taifa kuweka kambi shuleni, utaratibu uandaliwe wazazi wafaamishwe namna ya kuchangia, watoto wa kike waliopanga mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu shule iangalie namna ya kuwasaidia kukaa shuleni.
kiufupi, kikao kilikwenda vizuri sana, kama ulikosa hayo ndo baadhi ya yaliyokubaliwa na wazazi wa watoto, hivyo tazama picha zifuatazo kujionea hali halisi ya kikao:
Wazazi waliohudhuria kikao
Meza kuu, kutoka kushoto, Mratibu Elimu kata, Afisa Tarafa,
Katibu Wilaya CCM, Afisa Elimu Sekondari Wilaya,
Mkuu wa Shule, Mwenyekiti wa bodi, Afisa Mtendaji Kata,
mjumbe wa bodi
Ktibu wa Wilaya CCM, akijitambulisha
Afisa mtendaji Kata akichangia
Mwenyekiti wa bodi, akifafanua jambo
Mzazi akichangia
Kutoka kushoto, Katibu CCM Wilaya,
Afisa Elimu Sekondari na Mkuu wa Shule
wakisikiliza kwa makini
Mzazi akichangia
Mzazi akichangia
Mzazi akichangia
Mzazi akiendelea kuchangia
Mzazi akichangia
Mjumbe wa bodi, Mch. Elisante Mwinyigoha
akichangia jambo
Afisa Elimu Sekondari akisisitiza jambo
Wazazi wakiendelea kuchangia
Mwenyekiti wa bodi, ambaye ndiye alikuwa
mwenyekiti wa kikao akihairisha kikao
UONGOZI WA SHULE UNAWASHUKURU WAZAZI NA VIONGOZI WOTE WALIOHUDHURIA KIKAO HIKI, TUNAOMBA TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUIJENGA SHULE YETU NA KUINUA TAALUMA YA WATOTO WETU
No comments:
Post a Comment