Tuesday, October 29, 2013

Matokeo ya wanafunzi wa sekondari yataanza kupangwa kwa kutumia COURSE WORK zao!

Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa ameliambia gazeti la Habari Leo kuwa Serikali itabadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya Sekondari ili kazi anazofanya mwanafunzi shuleni, zitumike katika kumpatia alama ya ufaulu katika mtihani wa mwisho, mfumo unaolandana na ule unaotumika katika Vyuo Vikuu.
 
 
Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni yao kabla ya kuanzisha mfumo huo. Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini pia.
 
 
Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.
 
 
Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:
 
 
“Hatutaki kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya 0-34"
 
Chanzo: Habari Leo

No comments:

Post a Comment