Saturday, August 16, 2014

MWANZI YALALA YAKANDAMIZWA 3:1 NA KILIMATINDE, SASA KUWASUBIRI ITIGI SEC.


Na. Mwl. Venance F.
Timu ya mpira wa miguu ya shule ya sekondari Mwanzi imeshindwa kufua dafu mbele wenzao wa Kilimatinde katika mtanange uliopigwa jana ijumaa katika shule ya sekondari Kilimatinde. Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa shule ya sekondari kilimatinde ilikuwa mbele kwa mabao 3:1
Mchezo huo ulianza  saa 11:00 jioni kwa kuchezwa dakika 30 kwa kila kipindi, hadi timu hizo zinakwenda mapumziko mabao yalikuwa ni 1:1
Mambo yalikuja geuka kipindi cha pili kwa timu ya mwanzi kuongezwa mabao mengine mawili na hivyo kuhitimisha mtanange huo kwa Kilimatinde kuibuka washindi kwa 3:1.

walimu kama wanafunzi wao

Katika hali isiyotarajiwa timu ya walimu wa Mwanzi nao walitandikwa mabao kama waliyotandikwa wanafunzi wao. Mchezo huo kati ya walimu wa Mwanzi Sec. Na wenzao wa Kilimatinde ndiyo ulikuwa mchezo wa kwanza kuanza kabla ya ule wa wanafunzi, hadi mpira unaisha walimu wa Mwanzi walilala kwa mabao 3:0.

wasichana Mwanzi wajitutumua 

Timu ya netball iliwafuta machozi Mwanzi Sec kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 12 kwa 11, mchezo huo uliokuwa wakuvutia kila pande zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu, lakini mpaka mpira unaisha Mwanzi Sec. Waliibuka washindi kwa vikapu 12:11.
Kilimatinde wadaiwa kuchezesha mamluki
Katika hali isiyotarajiwa timu ya walimu wa Kilimatinde ilionekana kuchezesha wachezaji mamluki, madai haya yaliibuka baada kuonekana mchezaji mmoja wa timu hiyo kuonekana amenyoa mtindo wa kiduku, na kama inavyofahamika kwa maadili ya kazi mwalimu hawezi kunyoa nywele zake kwa mtindo huo, hata hivyo kulikuwa na madai mengine kuwa kilimatinde ilicheza walimu wengine kutoka shule ya Sekondari St. John na hivyo walimu wa Mwanzi kujigamba kuwa walicheza na shule mbili.
MATUKIO KATIKA PICHA
                                                    Kikosi cha walimu wa Mwanzi Sec.

                                              Kutoka kushoto Mwl. Varelian wa Kilimatinde na
 Mwl. Venance wa Mwanzi Sec. 

                                          Mwl. Emanuel {Second Master} akitoa maelekezo
 kwa walimu wake

                                       Walimu wakipambana uwanjani, mwenye jezi nyekundu
 namba 10 ni mwalimu wa Kilimatinde aliyezua sokomoko
kuwa ni mamluki cheki kiduku hicho ndicho kilichozua utata

                                          Mkuu wa Shule ya Mwanzi, Lubasi J. akitoa
                         maelekezo pembeni yake kulia ni mwl. Melesi {Second Master K/tinde}

                                             Kikosi cha wanafunzi mwanzi sec wakipiga dua
                                                                    Wakipiga tizi
                                     Refa alikuwa mwalimu Moris hapo akiwapa maelekezo
                           kikosi cha Mwanzi wenye njano, waliovalia nyekundu ni wa Kilimatinde

                                                   kikosi cha wasichana Mwanzi Sec

kikosi cha mwanzi sec wanafunzi

 Habari na picha na mwalimu Venance F.

Thursday, August 14, 2014

MWANZI SEC. KUUMANA NA KILIMATINDE KESHO IJUMAA

Na. Mwl. Venance F.
Moja ya kikosi hatari cha mwanzi kilichocheza
 na Chikuyu Sec. miaka ya nyuma

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwanzi kufanya ziara ya kitaaluma na michezo katika shule ya sekondari Kilimatinde, katika Ziara hiyo michezo mbalimbali itachezwa. Mwalimu wa Michezo wa Mwanzi Sekondari, Mwl Mwaigonela akitoa ratiba ya ziara hiyo kwa www.mwanzisec.blogspot.com alisema kuwa kabla ya mechi hizo kucheza kutatanguliwa na mdahalo kati ya wanafunzi wa shule hizo, itafuatiwa na mechi kati ya walimu wa Mwanzi Sec. na walimu wa Kilimatinde Sec. na baadaye kuhitimishwa na mechi za wanafunzi.

Akielezea maandalizi ya ziara hiyo, mwalimu huyo alisema kuwa, taratibu zote zimewekwa sawa, wanafunzi wa Mwanzi wana hali ya kuibuka washindi katika michezo yote iliyopangwa kufanyika, huku walimu nao wakiahidi kuwafundisha soka walimu wenzao wa Kilimatinde.

Mwalimu wa Zamu, Mwalimu Sylvery Hussein akiwatangazia wanafunzi wake aliwataka wakajiandae na safari ya kesho, na pia wasisahau kubeba vifaa vya michezo bila kusahau sahani za chakula chakula kitatolewa huko huko kwa wanafunzi wote ili kuhakikisha Kilimatinde wanapewa dozi za maana.

Mungu ibariki Mwanzi Sec. 

Tuesday, October 29, 2013

Matokeo ya wanafunzi wa sekondari yataanza kupangwa kwa kutumia COURSE WORK zao!

Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa ameliambia gazeti la Habari Leo kuwa Serikali itabadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya Sekondari ili kazi anazofanya mwanafunzi shuleni, zitumike katika kumpatia alama ya ufaulu katika mtihani wa mwisho, mfumo unaolandana na ule unaotumika katika Vyuo Vikuu.
 
 
Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni yao kabla ya kuanzisha mfumo huo. Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini pia.
 
 
Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.
 
 
Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:
 
 
“Hatutaki kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya 0-34"
 
Chanzo: Habari Leo

Sunday, October 20, 2013

MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE 2013 MWANZI SEC.

Wahitimu wa Kidato cha nne 2013 wakiingia ukumbini
 
Wahitimu kidato cha nne 2013 wakiwa wakijiandaa kuketi
 
Mkuu wa Shule, Mwl. Ntiruka akiwatambulisha na
kuwakaribisha wageni
 
Wanafunzi wa kidato cha tano Mwanzi Sec. wakitoa buradani 
 
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wakifanya Comedy

Wahitimu wakisoma risala mbele ya mgeni Rasmi
 

 
Wahitimu wakiwafuatilia wenzao wakisoma risala

Wahitimu wakitoa burudani

 Vijana wakishusha mistari ya nguvu
 

Wanafunzi wa kidato cha tatu wakishusha burudani ya kufa mtu
 

Mgeni rasmi, kaimu Mkurugenzi Mzee Masumbuko
akitoa hotuba yake
 
Mwanafunzi akichukua zawadi kwa kufanya vizuri darasani

Mwanafunzi wa kidato cha pili akichukua zawadi
kwa kufanya vizuri darasani

Mwanafunzi akichukua zawadi kwa kufanya vizuri darasani
 
Mwanafunzi akichukua zawadi kwa kufanya vizuri darasani
 
Muhitimu wa kidato cha nne akitunukiwa cheti chake
 
Wahitimu wakiimba shairi

Mmoja wa wahitimu akiwa pamoja na mama yake akionesha cheti
 

  
Mambo ya zawadi na keki hayo
 
Diwani Masabuni wa pili kushoto na viongozi wengine
wakipata msosi
 
 
Imeandaliwa na Mwalimu Venance F.
 

Tuesday, October 1, 2013

HALI ILIVYOKUWA KATIKA KIKAO CHA WAZAZI MWANZI SEKONDARI


Mwl. Venance F.
Leo katika Shule yetu ya Mwanzi, tulikuwa na kikao na wazazi wa watoto wanaosoma shule hii, lengo lilikuwa kukajadili maendeleo ya watoto wao, ya kitaaluma, nidhamu, utotoro na mengineyo, miongoni mwa waliohudhuria ukiachana na walimu wa Mwanzi, ni pamoja na Afisa Elimu Sekondari, Katibu CCM wilaya, Mratibu Elimu kata, Afisa Tarafa, Afisa Mtendaji Kata, Mwenyekiti wa bodi, na mjumbe wa bodi, wazazi waliazimia mambo mengi, miongoni mwa maazimio yalikuwa ni, wazazi kuchangia chakula ili watoto wao wawe wanapata chakula hapa shuleni, wazazi kuchangia ujenzi wa bweni [kumalizia bweni lililopo ambalo limefikia kwenye linta]  na uzio wa shule, [hili ni mpango wa muda mrefu], kuchangia ujenzi wa maabara chumba kimoja,  pia watoto wanaokabiliwa na mitihani ya taifa kuweka kambi shuleni, utaratibu uandaliwe wazazi wafaamishwe namna ya kuchangia, watoto wa kike waliopanga mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu shule iangalie namna ya kuwasaidia kukaa shuleni.
kiufupi, kikao kilikwenda vizuri sana, kama ulikosa hayo ndo baadhi ya yaliyokubaliwa na wazazi wa watoto, hivyo tazama picha zifuatazo kujionea hali halisi ya kikao:
Wazazi waliohudhuria kikao
                              Meza kuu, kutoka kushoto, Mratibu Elimu kata, Afisa Tarafa,
                                     Katibu Wilaya CCM, Afisa Elimu Sekondari Wilaya,
                                 Mkuu wa Shule, Mwenyekiti wa bodi, Afisa Mtendaji Kata,
                                                                    mjumbe wa bodi

Ktibu wa Wilaya CCM, akijitambulisha

                                                        Afisa mtendaji Kata akichangia

                                               Mwenyekiti wa bodi, akifafanua jambo

 Mzazi akichangia
Kutoka kushoto, Katibu CCM Wilaya,
Afisa Elimu Sekondari na Mkuu wa Shule
wakisikiliza kwa makini





                                                                   Mzazi akichangia

                                                                    Mzazi akichangia

                                                                  Mzazi akichangia


                                                     Mzazi akiendelea kuchangia

                                                                    Mzazi akichangia

                                              Mjumbe wa bodi, Mch. Elisante Mwinyigoha
                                                                     akichangia jambo


                                              Afisa Elimu Sekondari akisisitiza jambo

                                                    Wazazi wakiendelea kuchangia

Mwenyekiti wa bodi, ambaye ndiye alikuwa
 mwenyekiti wa kikao akihairisha kikao

 UONGOZI WA SHULE UNAWASHUKURU WAZAZI  NA VIONGOZI WOTE WALIOHUDHURIA KIKAO HIKI, TUNAOMBA TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUIJENGA SHULE YETU NA KUINUA TAALUMA YA WATOTO WETU